You are currently viewing Nguvu Ya Mnunuzi na Muuzaji

Nguvu Ya Mnunuzi na Muuzaji

Nguvu Ya Mnunuzi na Muuzaji

Kwenye biashara kuna nguvu zinazo husika kwenye kuamua ni nani kati ya mnunuzi au muuzaji ndio ana ushawishi zaidi juu ya mwenzake.

Nguvu ya Mnunuzi (Buying power).

Hii ni nguvu aliyo nayo mteja juu ya muuzaji. Nguvu hii inamruhusu mteja kuwa na Uhuru zaidi kwenye kufanya maamuzi ya kununua.

Nguvu ya Muuzaji (Selling power).

Hii ni nguvu aliyonayo muuzaji juu ya mteja. Nguvu hii inamfanya muuzaji kuwa na Uhuru zaidi kwenye kufanya maamuzi ya kumuuzia mteja.

Mfano Wa Buying Power Kubwa

Mteja anapokuwa na sehemu nyingi zaidi za kupata huduma ambayo muuzaji anatoa. Hii inampa Uhuru wa kukataa huduma maana anajua anaweza kupata huduma hio sehemu nyingine.

Mfano Wa Selling Power Kubwa

Pale ambapo huduma inayotolewa ni nadra, aidha kwa upatikanaji, gharama, au Ubora. Hii inampa Uhuru zaidi muuzaji kuamua jinsi ya kutoa huduma husika.

“With great power, comes great responsibility”

Uncle Ben, Spiderman

Mbali na nani mwenye nguvu kubwa zaidi, ni muhimu kukumbuka kwamba, jinsi nguvu hio inavyotumika ndio thamani halisi. Usitumie vibaya Nguvu uliyo nayo.

Je unahisi ipi ni kubwa zaidi kwenye Biashara yako, buying power au selling power?