You are currently viewing Maana Halisi Ya Mshindani Kwenye Biashara

Maana Halisi Ya Mshindani Kwenye Biashara

Maana Halisi Ya Mshindani Kwenye Biashara.

Mwaka jana, kuna wakati tuliongelea kuhusu ushindani kwenye biashara. Wakati huo, tiliona kuna changamoto kwenye uelewa wa watu juu ya maana halisi ya mshindani kwenye biashara. Tuangalie tena maada hii…

Wengi Tunavyofikiri.

Kwa haraka haraka, tukiambiwa, ‘Mshindani kwenye biashara’, tunaanza kufikiria biashara zote ambazo zinafanana na biashara zetu.

Ni Kweli.
Biashara zinazo fanana na biashara zetu, ni washindani wetu. Lakini ushindani kwenye biashara unaenda zaidi ya hapo.

Maana Ya Mshindani Kwenye Biashara.
Kitu au mtu yeyote atakaye mfnaya mteja asije kwako, kupata huduma.

Kwa Mfano.

Mgahawa na Gym.

Mteja wa gym anaweza kushauriwa asiende mgahawa fulani kula kitu fulani ili apunguze uzito.

Daycare na Dada Wa Nyumbani.

Kuna wazazi ambao kweweka mtoto daycare, ni kwaajli ya kuvuta muda wakati wako kazini, Dada wa nyumbani anakuwa nafuu zaidi kuliko hata daycare.

Nyumba za Ibada na Bar.

Nyumba za ibada zinaweza kuwasisitiza waumini wasiende kwenye Bar, na Bar zinaweza wafanya waumini wajishtukie kwenda kwenye nyumba za ibada.

Hospitali na Tiba Mbadala.

Wanaoamini kwenye matumizi ya tiba mbadala kama waganga wa kienyeji, wanaweza wasione haja ya kwenye hospitali, na wanaoenda mahospitalini wanaweza wasitake kwenda kutumia tiba mbadala.

Mabenki na Makampuni ya Simu.

Mteja anaweza amua kuweka hela benki, au kutunza tu kwenye simu kama kwenye Mpesa, Halopesa nk

Je aina gani ya biashara ni mshindani wako?