Makosa Ma5 Kwenye Kuanzisha Biashara
Kuna tafiti ilifanyika kuhusu maisha ya biashara ndogo, majibu yaliyo toka yalionyesha kwamba 98% za biashara zina kufa ndani mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Haya ni baadhi ya makosa yanayo fanyika wakati wa kuanzisha biashara hizi.
1. Kutokufanya Utafiti
Waanzilishi hawachukui muda kufanya utafiti juu ya biashara wanayo taka kuanzisha. Hii inapelekea kuongeza uwezekano wa biashara kufeli.
2. Kuajiri Haraka
Waanzilishi wanakimbilia kuajiri watu, bila kuwa na mpango mkakati wa kumudu mzigo unao ongezeka juu ya biashara pale waajiriwa wakiwa wengi.
3. Kuto Kutunza Kumbukumbu
Hii ni moja ya sababu kubwa inayo ua biashara nyingi. Biashara haitunzi kumbukumbu za matumizi, mahitaji, na taaarifa mbalimbali za uendeshaji. Hii inasababisha kushindwa kujua afya halisi ya biashara.
4. Kutokujua Sheria
Kuna biashara zinazojikuta zina kwama kwa kuto kufuata sheria husika, na mwisho wasiku kujikuta na faini nyingi, na kushindwa kuendelea.
5. Kutomuelewa Mteja
Hii pia inaonekana mara kwa mara, pale ambapo biashara inaendeshwa bila uelewa wa ndani zaidi wa soko husika. Mteja anabadilika, na kuto kumuelewa inaweza sababisha biashara kufa haraka.
Kosa gani kati ya haya umejikuta umefanya?